Baada ya miezi sita mume akafanyiwa hivi
Wednesday, February 5, 2014
I.... Na Christopher Lissa Katika hali isiyo ya kawaida, mwanamke mmoja aliyefahamika kwa jina la Pili Mohamed mkazi wa Buza, Temeke jijini Dar es Salaam anadaiwa kumfanyia unyama mzito mumewe Bw. Mohamed Ally kwa kumwagia maji ya moto mwilini baada ya mwanaume huyo kumfumania mkewe akiwa na mwanaume mwingine kitandani kwake. Mwanaume huyo amelazwa katika Hosipitali ya Wilaya Temeke huku akiwa amejeruhiwa sehemu kubwa ya mwili wake kutokana na kuunguzwa na maji ya moto. Akizungumza kwa taabu Wodini Hosipitalini hapo, Mohamed alisema kuwa ndoa yake na Pili imedumu kwa kipindi cha miezi sita tu ambapo ilianza kukumbwa na migogoro ya hali ya juu huku Pili ambaye anamiliki maduka ya dawa jijini Dar es Salaam akimdharau kwa madai kuwa hana uwezo hivyo kuanza kumnyanyasa. "Kabla ya siku ya tukio nilipewa taarifa kuwa mke wangu kila ninapotoka nyuma anaingiza mabwana ndani. Siku ya tukio niliamua kufanya mtego nilijifanya kuondoka, baada ya muda mfupi nmikarejea. Kweli nilivyogonga mlango kumbe mke wangu yupo chumbani na Pili akiwa na mume mwingine. Aliniuliza we nani? Nilimjibu mimi ni mumeo? Akanijibu mimi sina mume! Baada ya majibizano kidogo Pili akaja kunifungulia. Ghafla niliona mwanaume akichomoka kutoka ndani ghafla na kwa kasi ya ajabu na kutokomea. Nilishituka sana na kupigwa na butwa" alisema Mohamed. Alisema" Wakati nikiwa nimeduwaa, mke wangu akafunga tena mlango.Nilianza kugonga kwa fujo lakini hakufungua. Aliendelea kuongea ndani kwa matusi na maneno ya dharau. Muda mfupi akaja kunifungulia. Ghafla nilijikuta nikiwagiwa maji ya moto mwinini. Alinimwagia mara mbili. Nikaanza kukimbia hovyo.Yaliniunguza sana. Ngozi ilianza kuumuka na kudondoka"alisema Mohamed huku akijisikia maumivu makali. Mohamed amesema kuwa walikuwa katika hali ya kutokuelewana na mkewe baada ya mwanamke huyo kuanza kuwa na mahusiano nje ya ndoa. Shuhuda wa tukio hilo, Godfrey Peter alisema kuwa, kabla ya kufanya tukio hilo Pili aliwapigia simu upande wa mwanaume kuwa wafike nyumbani kwake kwaajili ya kushuhudia tukio ambalo atamfanyia mumewe. "Naona wakati akipiga simu alikuwa amejifungia ndani akichemsha maji kwenye bilika la umeme 'Hita'.Nilipo fika tu nilikuta Mohamed akimwagiwa maji.Pili alisema nakudai talaka yangu kwanini hunipi?Mimi nimekwambia sikutaki!" alisema Godfrey akimnukuu Pili. Alisema alichokifanya ni kumpa huduma ya kwanza majeruhi ambaye tayari nyama zilianza kunyofoka, walimpeleka kituo cha Polisi kisha Temeke Hosipitali ambako alilazwa na kutolewa kesho yake kabla ya hali kubadilika na kurudishwa tena Hosipitali hapo. Shemeji wa majeruhi Yusra Mussa aliliambia Sani kuwa baada ya kufanya tukio hilo Pili alikwenda kituo cha Polisi Chang'ombe na kutoa taarifa za uongo kuwa amevamiwa nyumbani kwake na mtu asiyemfahamu. "Aliongopa kuwa amevamiwa na mtu asiyemfahamu. Tulipokwenda sisi kutoa taarifa Polisi walishangaa baada ya sisi kudai kuwa Pili ndiye aliyemfanyia unyama mumewe. Ilibidi tupeleke uthibitisho pale kuwa pili na mohamed ni mke na mume.Inasikitisha sana. Huyu mwanake sijui anaroho ya aina gani" alisema Yusra. Alisema cha kushangaza zaidi siku ile ile ya tukio Pili alifika nyumbani kwa ndugu wa mumewe kudai baadhi ya vitu vyake akiwa na mjumbe, huku akidai hajari kabisa hali ya mumewe. "Alikuja kudai vitu vyake.Tulimhsihi kuwa asubiri mumewe ashughulikiwe kwa matibabu lakini aligoma kuondoka na kudai lazima apewe vitu vyake. Baada ya hapo akatishia kwenda Polisi kuchukua askari ili waende nyumbani kwa mumewe kuchukua vitu kinguvu. Alivyo fika Polisi akawekwa chini ya ulinzi baada ya madai yake kuwa amevamiwa na mtu asiyemfahamu kubumbulika na kuwa kumbe ni mumewe wa ndoa na alifumaniwa" alisema Yusra huku akiulamu vibaya upende wa ndugu wa mwanamke kutokutoa ushirikiano katika suala la mhonjwa. Baadhi ya ndugu na majirani wameomba vyombo vya dola na sheria pamoja na dawati la ukatiliwa kijinsia kuingilia kati suala hilo ili kuhakikisha kuwa sheria inachukua mkondo wake kwani Pili alisikika akijinasibu kuwa Pesa itaongea. "Muda mfupi mkewe akamwita bwanaake mwingine ndani kwake. Wakiwa katika faragha chumbani wakiivuruga amri ya sita mume alirudi nyumbani ghafla na kuanza kugonga mlango.Mke aliuliza kwa ndani ni nani aliyekuwa anagonga mlango
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment