INASIKITISHA SANA
Na Christopher Lissa
Hakika Dunia
inaelekea ukingoni. Mwanaume mmoja ambaye
aliyefahamika kwa jina la
Atanasi Kimani mkazi wa eneo la
Mbondole Kivule, Ilala jijini Dar es Salaam anayedaiwa alikuwa ni mchungaji wa
kanisa la Evangelical Assemblies of God (EAGT) huko Dodoma, anashiliwa na Jeshi
la Polisi kanda maalumu ya Dar es Salaam kwa tuhuma za kuishi kinyumba na binti
yake wa kumzaa mwenye umri wa miaka 16(jina linahifadhiwa).
Habari za uhakika
ambazo zimefuatiliwa kwa kina na Sani
zimetonya kuwa, Atanasi alianza kumuingilia binti yake tokea akiwa darasa la
tatu ambapo sasa binti huyo yuko darasa la saba.
Baada ya kupata
taarifa hizo Sani lilifika nyumbani kwa Mzee Atanasi na kuongea na mkewe, binti
aliyekuwa akifanyiwa unyama huona majirani ambao walielezea kulaani vikali
uchafu wa Atanasi.
Akisimulia jinsi
tukio hilo lilivyobumburuka, mke wa Atanasi
Bi. Tumaini Kabeja alisema kuwa
binti aliamua kuanika ukweli siku
ya Januari 21 mwaka huu baada ya kuingiliwa na baba yake alfajiri.
"Nimeishi na
mzee Atanasi kwa muda wa miaka miwili sasa pamoja na binti huyu. Huyu binti ni
mtoto wa mke mwingine ambaye waliachana. Mimi ni mama yake wa kambo.Hata hivyo
nilikuwa sijui lolote linaloendelea baina yao ndani, kwa sababu binti ni
mdogo.Kumbe mume wangu ameanza kumwingilia mwanaye miaka mingi iliyopita na
alikuwa akimtishia kuwa akitoa siri atamuuwa"alisema Bi, Kabeja.
Bi. Kabeja
alisema kabla ya kumuoa Atanasi alikuwa
akiishi na watoto wake wawili binti aliyekuwa anabakwa na mwingine wa kiume
lakini alimtimua mtoto wake wa kiume ili aweze kupata nafasi ya kuvuruga amri
ya sita na binti yake.
"Baada ya kunioa
mimi nasikia aliacha kutembea na mwanaye.Lakini alikuwa na wivu mno. Hakutaka
binti atoke. Alikuwa akipmiga sana. Nilikuwa sijui kwanini? Kumbe alikuwa
amemfanya mke mwenzangu. Masikini!" alisema Bi. Kabeja kwa masikitiko.
Aliongeza "Siku
ya tukio, yaani Januari 21,mimi huwa nafanya bishara ya kuuza kachori shule ya
msingi Mbondole, kumbe kila nikiondoka alfajiri baba mtu humfuata binti yake
sebureni na kumuingilia hadi anaporidhika. Siku hiyo binti alipata maumivu sana
ilibidi aniambie tu kuwa eti ni mwambie baba yake aache tabia chafu ya kumbaka.
Nilishituka sana. Nilimhoji ndipo aliponisimulia kila kitu.
Siku hiyo hiyo
nilimpeleka Polisi Staki Shari kutoa taarifa na tukaelekea Hosipitali ya Amana.Nilikutana na watu wa
Ustawi wa Jamii baada ya kujiridhisha na
maelezo yangu na ya mtoto tukafanya
mtego wa kumnasa mtuhumiwa ambapo mimi
nilijifanya nimelazwa hapo baada ya kuzidiwa. Alikuja mtuhumiwa akakamatwa na
baada ya kumbana sana alikili kulala na mwanae ingawa alisema mara moja
tu" alisimulia Bi. Kabeja na kwamba mumewe alikuwa ni mchungaji wakati
akiishi Dodoma na nimaarufu kwa jina la mchungaji hadi sasa.
Sani liliweza kuongea
na binti aliyekuwa akifanyiwa ukatili huo ambaye alikiri kuanza kulala na baba
yake tokea akiwa darasa la tatu.
"Sijawahi kulala
na mwanaume mwingine isipokuwa baba. Tokea baba alipoachana na mama kule Dodoma
alituchukua mimi na kaka. Tukawa tunaishi Mbagala. Alipanga chumba kimoja na
Sebure. Usiku alikuwa akitaka niwe na lala naye na kaka anabaki Sebureni.
Alikuwa ananifanyia mambo ya ajabu sana. Alikuwa akiniziba mdomo ili nisipige kelele. Nilikuwa nasikia maumivu
makali mno lakini alikuwa akinitishia kuwa nisema ataniuwa"alisimulia
binti huyo.
Alisema"
Aliendelea kulala na baba yake hadi walipohamia eneo la Mbondole, hapo baba
yake alimfukuza mtoto wake wa kiume ili
apete nafasi ya kulala naye, hadi alipomuoa Bi. Kabeja. Alisitisha kidogo
kulala na mimi baada ya kuoa. Alianza tena kulala na mimi baada ya mama kupata
uja uzito. Kuna kipindi alikuwa akiniingilia nyuma.Hadi Januari 21 ambapo
nilichoka na kuamua kumueleza mama. Nilikuwa naogopa kwa sababu baba ni mkali
sana.Huwa anatupiga sana mimi na mama na kutishia kutuuwa kwa panga"
Binti huyo alisema
kutokana na kutumika sana kimapenzi na baba yake hivi sasa yuko sugu licha ya
kuwa naumri mdogo.
"Naiomba
Serikali iingilie kati kulishughulikia suala hili, maana baba akiachiwa
atatuchinja mimi na baba.Niko darasa la saba hivyo nahitaji kusoma na kufauri
ili niweze kutimiza malengo yangu"alisema Binti huyo kwa uchungu.
Mjumbe wa shina namba
25 katika eneo hilo Cosmas Manyota
alithibitisha kupokea taarifa za tukio hilo la kusikitisha na kwamba sheria
lazima ichukue mkondo wake.
"Huyu jamaa
kwanza muda wote yeye ni mtu wa hasira. Hana uhusiano mzuri na wenzake. Yeye ni panga mkononi.
Watoto na mkewe alikuwa anawapiga vibaya mno"alisema Manyota.
Familia hiyo imeomba
msaada wa hali na mali kwa wasamalia wema kutokana na kuishi maisha magumu
baada ya baba yao kutiwa mbaroni.
"Yeye ndiye
alikuwa mtafutaji, lakini kutokana na unyama aliokuwa ameufanya tuliona ni vema
tuteseke tu yeye aende ndani. Hatuna kitu hapa. Tunakula kwa taabu sana.
Mwanangu huyu aliyekuwa anabakwa yuko darasa la saba. Anajiandaa na mitihani.
Tunaomba msaada kwa watanzania wenzetu. Hata hivyo mimi najitahidi kuuza
kachori lakini haikidhi mahitaji.Tusaidieni"alisema Bi. Kabeja na kwamba
mtu yoyote anayehitaji kuisaidia familia hiyo awasiliane nayo kwa namba
0756701134 au awasiliane na mwandishi wa habari hizi kwa namba 0654 586788 ama
afike ofisi za gazeti hili mtaa wa Shauri Moyo na Lindi Ilala Jijini Dar es
Salaa au awasiliene na mtangazaji wa kipindi cha hatua Tatu cha Redio Times FM
Edson Mkisi Junior kwa namba 0718377080.
Shime Watanzania kutoa kwako ni kuchangia jitihada za kupinga
ukatili wa kijinsia kwa watoto.
BINTI ALIYEKUWA AKIBAKWA NA BABA
No comments:
Post a Comment