Saturday, June 9, 2012

SOMA NICHEKELEE ZA KUVUNJA MBAVU AMBAZO HUWEZI KUZIPATA MAHALI POPOTE!

JAMAA ACHEMKA !!
Jamaa mmoja aliambia atoe historia fupi ya marehemu msibani akasimama na kusema wanamsiba oyeeee!!! Halafu akaendelea kusema hivi: “Unajua kilichompata marehemu? Jaribu nawe siku moja uone.
Duh watu wote wakabaki kimya kwa mshangao uliojaa huzuni!!


NITAKUJA KESHO!!

Mchawi mmoja kutoka kijiji cha Sumbawanga alikuwa anasumbuliwa na magonjwa sugu ilibidi aende Kwa Mchungaji ‘Babu’ Loliondo. Alipofika Babu bila kujua kama jamaa ni mchawi
Babu: Karibu
Mchawi: Asante
Babu: Kabla ya kunywa dawa tunaanza na maombi.
Mchawi: Kama ndiyo hivyo basi nitakuja kesho.
Hiyo ni balaa


JIFUNZE METHALI ZA KIHINDI!!
Methali : Nyani haoni
Jibu: Varisa miwani
Methali: Debe tupu
Jibu: Weka dengu ama choroko
Methali: Maskini akipata
Jibu: Iko acha iba katika jumba ya watu
Methali: Simba ikizidiwa
Jibu: Iko kaa chini pumzika
Methali: Penye kuku wengi
Jibu: Chinja bili tatu
Methali: Asie sikia la mkuu
Jibu: Peleka Takukuru
Methali: Penye wengi
Jibu: Iko kutano ya CCM


BABA NA MWANA!!
Mzazi mmoja alikuwa akiongea na mwanae na mazungumzo yao yalikuwa kama hivi:-
Baba: Mwanamgu shika hii pesa Sh. 500/= usimwambie mama yako kama nimelala kwa housegirl
Mtoto: Tatizo wewe baba mbakhili mama alipolala na dereva kampa 1000/=
Baba: Eee….unasema vipi?


MWALIMU NA MWANAFUNZI!!
Mwalimu: Ikiwa kuku ni jamii ya ndege, je samaki ni jamii ya nini?
Mwanafunzi: Aaah mbona raisi sana mwalimu ni jamii ya meli
Mwalimu: Mmmh hili darasa hili sina hamu nalo

5 comments: