Manaiki ambae ametamba sana kwenye video yake ya nafanya mambo na sasa ameachinia ngoma yake mpya aliyoiita jina la "Twende Sawa" ambayo sasa imeanza kuwa gumnzo amesema" Kun wimbo wangu ambao nilikuwa najipanga kumshirikisha Jose kwa vile yukp hapa nchini nitatumia furusa hiyo kufanyanae kazi ambapo nategemua kukutana nae muda wowote kuanzaia sasa" Alisema Manaiki.
Aidha mwanamuziki huyo aliongeza kusema Jose ni mwanamuziki bora duniani hivyo anaamini katika wimbo wake huo watafanya kitu flani cha kushangaza dunia kwani anauamini uwezo wake na wa Jose hivyo wimbo huo utafanya mapinduzi ya ukweli tu baada ya kuuachia hewani.

Mji wa Zanzibar July 6-7 unatarajia kulipuka kwa burudani ya kihistoria huku wasanii nyota nchini wanatarajia kufunika vibaya kwa burudani kabambe.
Onesho hilo lililoandaliwa na kamapuni ya Island Promotion linatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa Gymkahana siku ya tarehe 6/7/2012 huku wasanii wakongwe kama Joseph Haulu,Professa J, Bi Kidude,Offside Trick,Bery Black,Bay J,Aboyz, Man Tuzo,Rich Mavoko,Shamazee wakitatarajia kufunika vikali.
Aidha waratibu hao waliongeza kusema kuwa baada ya shoo hiyo ya Gymkhana siku itakayofuata yani tarehe saba sikukuu ya sabasaba kazi itamalizikia kwenye ukumbi wa Peruu Pub huku kiingilio kitakuwa shilingi elfu nne mlangoni ambapo mashabiki wameomba kuwahi ukumbini ili kupta nafasi za kukaa.
No comments:
Post a Comment