Tuesday, July 3, 2012

DEMU ALIYEKATALIWA MIMBA NA CHARLZ AJIFUNGUA MTOTO WA KIKE!

Msichana aliyewahi kuripotiwa na gazeti hili miezi ya hivi akaribuni kuhusu kulazimishwa ngono zembe na mwanamuziki na raisi wa bendia ya Mashujaa Charles Gabriela.k.a Charlz Baba aliyefahamika kwa jina la moja la Anita amejifungua mtoto wa kike aliyeitwa kwa jina la Genevivu Charles Baba.
Habari za uhakika zilizothibitishwa na msichana huyo ambae ni mtanzania mwenye asili ya Kenya zilisema baada ya mateso ya muda mrefu ya kulea mimba sasa Mungu amemjalia na kajifungua salama huku mtoto wake akija mwenye afya tele.
Aidha msichana huyo ambae gazeti hili liliwahi kuripoti akimlalamikia mwanamuziki huyo kwa kumfanyia unyama kipindi walipokutana kimwaili kwa kuchana kondomu makusudi hali iliyomfanya kupata ujauzito huo usiotarajia kisha mwanamuziki huyo kukataa kushirikishwa chochote kuhusu mimba hiyo.
Hata hivyo anita aliongoza kusema kuwa baada Charlz kupata taarifa za kujingua kwake kupitia rafiki zake huku wakimwambia kuwa mtoto kafanana na yeye hadi sauti Charlz alimpongeza kwa kujingua salama huku akisema anamtakia malezi mema mtoto wake huyo.
Hata hivyo Charlz mwenyewe alipotafutwa kuzungumzia tukio hilo hakupatikana baada ya kudaiwa alikuwa safari mkoani Singida na bendi yake ya Mashujaa, lakini jamaa wa karibu na mwanamuziki huyo walisema mtoto huyo kamuumbua Charlz kwani licha ya jinsia yake ya kike lakini anafanana nae kila kitu hadi sauti hasa akiwa analilia uji.

No comments:

Post a Comment