
Na Christopher Lissa, saninewz
Jeshi la Polisi mkoa maalumu wa Kipolisi Ilala, jijini Dar es Salaam umetoa amri kwa wanawake wote wanaofanya biashara halamu ya kuuza miili yao katika madanguro huku likieleza kuwa litafanya oparesheni nzito ya kusambaratisha madanguro hayo kisha kuwatia mbaroni wahusika watakao kaidi amri hiyo.
Kamanda wa Polisi Ilala, ACP Marietha Minangi ambaye ni mratibu mkuu wa maadhimisho hayo amesema kuwa jeshi lake limejipanga vyema kudhibiti sehemu zote zilizokubuhu kwa biashara ya ukahaba na kufunga madanguro yote ambayo kwa sasa yanatukuka kwa biashara halamu ya ngono.
"Tunataka kukomesha biashara hii kabisa mkoani kwetu.Tutaendesha Oparesheni kubwa sana ya kufunga madanguro, kutoa elimu na kuwakamata wahusika wote.Kwa hili hatutakuwa na msalie mtume. Nawataka wasichana wote wanaofanya biashara hiyo katika madanguro au sehemu yoyote kuacha kabla jeshi la opareshini hii haijawakumba"alisema RPC Minangi.
No comments:
Post a Comment