Mgomo wa madaktari wasabisha afungue wodi nyumbani kwake
Kijana mmoja ambae ni dereva tax Juma Mkalaki '34' amenusulika kufa baada ya kumwagiwa kalai nzima lenye mafuta ya yaliyokuwa yansubiri kutumbukizwa viazi ili zime chips.Akiongea kwa masikitiko makubwa Juma ambae anaishi Mburahati nyumbani kwao alisema tukio hilo lilitokea tarehe 25/ mwezi uliopita saa saba za machana maeneo ya Mwembe Chai.Juma aliendelea kusema kuwa alifika kwenye banda hili kwa ajili ya kupata chakula na wakati alipokaribia alikutano mabishano kati ya mkaanga chips na mteja mwingine.
Hata akiwa hana hili na lile alimuona mpika chips huyo akinyanyua kalai la mafuta akadhani kuwa ananyanyia ili aongeze mkaa lakini alishitukia amemwagia mafuta hayo yaliyokuwa yamechemka hadi kuwa mekundu.
Juma anaema alishtuka baadae alianza kupiga kelele za kuomba msaada"Kaka nilichanganyikiwa sana nikawa kama chizi ambapo nilianza kukimbia huku na kule kwa ajili ya kuomba msaada" Alisema Juma
Hata hivyo baada ya muda wasamalia wema walimkamata na kumpatia huduma ya kwanza kwa kumpaka dawa ya meno na baadae kumpelea polisi kwa ajili ya kuchukuwa pf3 ili wampeleke hospital ambapo polisi walimfungulia taarifa MAG/IR/11328/12 SHAMBULIO LA K/MWILI.
Aidha baada ya kupewa pf3 alipelekwa kwenye Hospital ya Magomeni kwa ajili ya matibabu lakini alikumbana na mgomo wa madaktari ambapo akiwa kwenye uchungu mkali alipelekwa kwenye hospitali ya Modern iliyopo Manzese.
Lakini hata hivyo dereva huyo anasema aliamua kulazwa nyumbani kwaje kutokana na mgomo huo, na amewapongeza madereva wenzake kwa kumlea kipindi chote kwani tangu aumie amekuwa akishirikiana nao pamoja mwanzo mwisho.
No comments:
Post a Comment