AMAN JAPHET NGUKU MTUNZI WA KITABU CHA SAFARI YA NDOTO AKIHUTUBIA WAKATI WA UZINDUZI WA KITABU HICHO KATIKA UKUMBI WA BEIJING JIJINI DAR ES SALAAM
HII NDIYO TAARIFA FUPI YA UZINDUZI
Vijana wa kitanzania wameaswa kuacha kulalamika na kuishi katika maisha ya nadharia, badalayake wameshauriwa kubadilika kuwa watendaji na wenye uthubutu wa kutimiza malengo yao.
Hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa Mtendaji wa Amajat Investment Bw. Aman Nguku katika uzinduzi wa kitabu chake kiitwacho SAFARI YA NDOTO kinachobeba kaulimbiu "Siyo Serikali ni Mimi, Wewe naSisi"
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Bw. Nguku alisema, imefika wakati sasawatanzania hasahasa kundi la vijana waamke kutoka usingizini na kutimiza malengo ya kimaisha ambayo wanapenda kufikia.
"Imetosha sasa kusema kesho, kufikiri bila kutenda na kuongea bila vitendo .Kinachotakiwa nikuanza utendaji" alinukuu Bw. Nguku kutoka katika kitabu chake chenye kurasa 108.
Akieleza madhumuni ya kuandika kitabu hicho, Bw. Nguku ambaye pia ni mwanafunzi wa mwakawatatu anayesomea shahada yaUchumi katika Chuo Kikuu cha Ardhi jijini Dar es Salaam alisema:
"Hiki kitabu ni mahususi kwa wale watu ambao wana ndoto mbalimbali katika maishayao lakini hawajui pakuanzia.Iwe ndoto ya kufanyabiashara maarufu , mwanasiasa au daktari bingwa.Hiki kitabu ni ramani kwako"
Aliendelea kusema"Kitabu hiki kinaweza pia kuwa changamoto kwa wale ambao wamekata tamaa katika maisha.Kwa kusoma maandishi ya kitabu hiki, wanaweza wakafufua ndoto zao na kufanikiwa katika yale waliyoyapanga"
Safari ya Ndoto pia inabeba dondoo kutoka kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, mfanyabishara maarufu Bw. Reginald mengi na Mkurugenzi wa Helvetic SolarContractors Bw. Patroick Ngowi.
Kitabu hiki kinasambazwa katika maduka mbalimbali jijini Dar es Salaamna nchi nzima ili watanzania wengi wapate kukisoma. Kinauzwa kwa Tsh.5000 tu
Kwa sas, mtunzi pia anaandika vitabu vingine viwili vyenye vichwa 'Ndogo lakinimuhimu,kesho' na What is Life for (Maisha ni ya nini)
Kwa mawasiliano na mtunzi
Aman Japhet Nguku o713818409.
No comments:
Post a Comment