Saturday, June 23, 2012

MAMA WEMA

WADAU SOMENI MAELEZO YA MAMA MZAZI WA WEMA SEPETU BI.MARIAMU SEPETU
HIVI NDIVYO ALIVYOFUNGUKA KWENYE RUNINGA YA CLOUDS TV
AKIWA KATIKA KIPINDI CHA TAKE ONE KINACHOANDALIWA ZA ZAMARADI MKETEMA YULE MISS MWANZA

"Na watu wengi watanzania wataweza kujiuliza kwamba kwanini nimemtaja Jack Wolper? Iimebidi nimtaje Jack Wolper kwa sababu ni mhusika.
Yeye ndiyo aliyezungumza kuhusu masuala ya Wema. Atampa Wema muvi acheze. Sababu aliona kwamba ni mzurulaji.
Sasa mimi namtaja yeye.Alitamka kwamba atampa muvi acheze ili aweze kununua kitanda.Ni sawa.Lakini kama mlivyoona, Wema hapa ni kwao.Hapa nilipo nimekaa nyumbani kwangu.
Sasa napenda nizungumze kwamba Jack siyo kwamba nimemtaja simpendi,Jack ni mwanangu na kila omba nisememtu ni mtoto wangu.Wasanii wote na watoto ambao nimewazidi umri ni mtoto wangu.
Imeniuma. mzazi unaposikia kwamba mtoto wako anasemwa kwamba ataweza kupewa muvi acheze, anunue kitanda.Wema siyo wakupewa muvi na Jack anunue kitanda.
Naomba Jack, na bado naendelea kukutaja.Wataokauchukia wanichukie na watakaosema na waseme, lakini bado mimi nazungumza.
Mimi huwa sipendi kumzungumza mtu chinichini au chini ya meza, namzungumzia wazi.
Utachukia utafurahi lakini nasema si tabia nzuri.Wasanii manapaswa mpendane, msaidiane, kwa jambo jema au lingine.
Kusemana semana hamtaweza kufika popote.Naomba muwe na upendo wa dhati siyo upendowa hapa na pale.
Weka kishasemwa na magazeti wewe ni mtoto wa kike wewe ni mtoto wa kike mnapaswa kukaa wote kwa pamoja.Lengo liwe moja muweze kusaidiana.
Siyo kwamba mi nakusema au Wema alikusema hata Irene pia aliweza kukuzungumza.Forcus your life.Angalia maisha yako unayapeleka vipi?Siyo uangalie maisha ya wenzio.Mwanangu asemwe na magazeti asemwe na wewe pia ukiwa ni mwanamke.
Wema alikuwa ni mpole sana.Actually mimi , Wema kama wema sikumnyonyesha mimi.Nilikuwa na Dasphones.Ilinisumbua sana kama miaka kama 15 hivi.
Nilipokuja kumzaaa yeye mimi nikafanyiwa oparesheni.Lakini baada ya mwezi mmoja na nusu.
Amekuwa,yaani wema alikuwa ni mtoto mmoja mpole, hapa mtaani kote kila mtu Wema alishatoka na kila mtu.
Alipofika miaka mitatu nanusu akawa na rafiki yangu.Yaani Wema anakuwa pale.Yeye anajua ni ka mama Wema.
Yaani Wema alikuwa ni mpole mbele za watu.Yaani Wema hakuwa na kitu chochote, lakini ukisha kaa na Wema utajua kuwa umetoka na mtoto.we mashalah mwenyezi Mungu lazima ukumbali.Lazima umkubali, lazima ukubali.Namshukuru mwenyezi Mungu. Unajua unapozaa mtoto hana kilema hana cha nini unamshukuru mwenyezi mungu kwa kweli.
Asante sana.Mimi sikutegemea kama Wema jinsi alivyokuwa atakuja kuwa miss Tanzania.Lakini ndo mambo yalivyo mpangia.
Lakini hakuna kitu chochote ambacho kilikuwa kinanionesha kwamba Wema arakuwa Miss Tanzania.
Wema ni mtoto wangu wa nne katika kuzaliwa. Na wema amesoma International School kuanzia Form one mpaka form four.
Kweli Wema alichukua umiss, ameingia kwenye umiss mwaka 2006, ingawaje kwa matatizo sana lakini tuliweza kumruhusu akachukua umiss Miss Tanzania.
Baada ya hapo kwa bahati nzurialikuwa miss kinondoni akawa mshindi wa pili.Baada ya hapo akachukua miss tanzania 2006 mpaka 2007.
Kumekuwa na matukio mengi toka wema amechukua umiss.Yaani kwa kweli nikiwa kama mzazi kwa siku ya leo kumuelezea Wema toka nimemzaa.Kwakweli nikiwa kama mzazi hasa mama.imekuwa inaniuma.Inafikia hatua mpaka nachanganyikiwa kuhusu magazeti kumuandika wema.
Lakini Wema kama Wema nilivyo mlea kwa malezi ya mama, nimemlea katika maadili ya kiafrika, nimemlea katika maadili mazuri na nimemlea kamani mtoto wangu.
Lakini wema amekuwa na matukio mbalimbali. Lakini matukio ya kawaida kwa mtoto.Siwezi kusema hawezi kutenda mambo kama haya"
Itaendelea

 
Maoni tuma sms 0654 5867 88 au E mail chrisslissa1981@yahoo.com usibip.

No comments:

Post a Comment