endwa Amina Chifupa wa Mpakanjia a.k.a Mama Rahmanino a.k.a Maboga.Aliyekuwa Mbunge wa vitu maalum CCM. Mtangazaji nyota wa Redio Clouds FM, muasisi wa kipindi cha Leo Tena kinachoongozwa na Dina Marious hadi sasa.Kipindi bora Tanzania na chenye mvuto.
Binafsi nilimpenda sana dada Chifupa.Nilizoea kumwita mpiganaji.Dada aliyejiamini kwa kila alichokuwa amepanga kukifanya.Atabaki kuwa mfano milele kwa vijana hasa wasichana wenye ndoto za kweli katika maisha yao.
Amina umeondoka dada yetu bado tunakukumbuka.Tunakumbuka busara zako na harakati zako katika mapambayo dhidi ya dawa za kulevya.Mungu ailaze roho yako maharipema peponi.Amina kama lilivyo jina lako.
Pia tunamuombea apumzike kwa amani mumeo Mohamed Mpakanjia 'Med Kitendawili'Hakika kimwili hamko nasi ila kiroho tuko pamoja.
Leo utasomewa kisomo nyumbani kwenu TPDC saa 10. Mimi nitakuwepooo!
R.I.P AMINA CHIFUPA & MPAKANJIA
No comments:
Post a Comment