Tuesday, June 19, 2012

BURIANI MPIGANAJI



Uongozi wa kampuni ya Watoaji wa Maandishi wa SANI, inayo huzuni kubwa kutoa salaamu zake za rambirambikwa familia, ndugu, jamaa na marafiki pamoja na waandishi wote wa habari nchini kwa kuondokewa na mpiganaji Willy Ogunde Edward, Mkhariri wa Gazeti la Jambo Leo.

Kwa ujumla wafanyakazi wa Sani tumepokea kwa masikitiko makubwa kifo hiki cha Willy.Tunatoa pole kwa wenzetu wa Jambo Leo, ambao tunaamini kuwa wako katika kipindi kigumu mno wakati huu wa majonzi.

Tuko pamoja katika msiba huu mkubwa ulioikumba tasinia yetu ya habari.


Atakumbukwa kwa ucheshi, Uchapakazi na uadirifu. Ikumbukwe kuwa amekumbwa na kifo akiwa kazini.Japo tulimpenda lakini Mungu amempeda zaidi.Bwana alitoa Bwana ametwaa jina lake lihimidiwe.

No comments:

Post a Comment