Thursday, May 24, 2012

MNYIKA ASHINDA KESI UBUNGO

Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam , leo imetoa hukumu katika kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi Mkuu jimbo la Ubungo jijini Dar es Salaam, ambapo Mbunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) John Mnyika ameshinda kesi hiyo.Kesi hiyo ilifunguliwa na aliyekuwa mgombea wa kiti cha Ubunge katika jimbo hilo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bi. Hawa Ng'umbi.Hukumu hiyo ilisomwa na Jaji wa Mahakama hiyo Bi. Upendo Msuya mapema hii leo ambapo pia mahakama hiyo ilimtaka Bi.Hawa kumlipa Mnyika gharama zote alizotumia katika kesi hiyo.Kufuatia matokeo hayo, mamia ya wafuasi wa CHADEMA waliokuwa wamefurika katika mahakama hiyo waliondoka kwa shangwe na vigeregere huku wale wa CCM wakibaki wakiwa hawaamini macho yao.Polisi waliimarisha ulinzi mkali mahakamani hapo

No comments:

Post a Comment