Monday, May 28, 2012

LULU APANDA KIZIMBANI MAHAKAMA KUU


Msanii nyota wa filamu nchini, Elizabeth Michael 'Lulu' leo kwa mara ya kwanza amepandishwa kizimbani katika Mahakama Kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akikabiliwa na tuhuma za mauaji ya aliyekuwa msanii nyota wa filamu Steven Kanumba.

Akiwa mahakama kuu suala la mjadala wa umri wake lilichukua mvutano mkubwa baina ya mawakili wa Serikali na mawakili wanaomtetea ambao walidai kuwa mteja wao anaumri wa chini ya miaka 18 na kwamba kesi yake isikilizwe na mahakama ya watoto huku wale wa Serikali wakidai Lulu anamiaka 18.Kesi hiyo iliahirishwa hadi Juni 11 mwaka huu ambapo mahakama hiyo itatoa uamuzi juu ya utata huo.

No comments:

Post a Comment